Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jalada la kesi ya mauaji lazua mjadala

50142 JALADA+PIC

Wed, 3 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Jalada la kesi ya mauaji namba 27 ya 2016 limezua mjadala katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala baada ya wakili wa Serikali kueleza kuwa lipo kwa mkuu wa upelelezi mkoa (RCO).

Baada ya wakili wa Serikali kudai lipo kwa RCO washtakiwa wamedai kuwa RCO alipotembelea gerezani walimuuliza na kuwaeleza halipo katika orodha ya majalada anayofanyia kazi na kwamba lililopo ni kesi ya mauaji namba 27 lakini la mwaka 2017.

Hayo yamejiri leo Jumanne Aprili 2, 2019 mbele ya hakimu Flora Mujaya na wakili wa Serikali, Grace Lwila ambaye alieleza Mahakama kesi ilipangwa kwa ajili ya kutajwa, upelelezi haujakailika na jalada lipo kwa RCO.

Kufuatia maelezo hayo, washtakiwa hao waliopo gereza la Keko na wengine Segerea walidai kuwa kwa nyakati tofauti RCO ilipotembelea gerezani walimuulizia kuhusu kesi yao.

Hata hivyo, aliwaambia kuwa jalada la kesi yao halipo kwenye orodha ya kesi zinazofanyiwa uchunguzi na kwamba iliyopo ni kesi ya mauaji namba 27/2017.

Mshtakiwa Salim Shaaban (34) maarufu White alidai kuwa aliongea na RCO alipotembelea gereza la Segerea kwa zaidi ya dakika 10.

Alidai alielezwa kuwa waliitafuta kesi yao ya mauaji namba 27/2016 kwenye orodha ya kesi ambazo wanazifanyia uchunguzi lakini haipo ila kuna ya mauaji namba 27/2017.

Baada ya kueleza hayo, wakili Lwila alidai kuwa anapata taarifa za upelelezi kutoka kwa mpelelezi wa kesi hiyo kuwa jalada lipo kwa RCO.

"Yeye ndiye mpelelezi wa kesi, kama ni hivyo RCO huyo hana taarifa sahihi na upelelezi wao," alieleza Lwila.

 Baada ya kusikiliza hoja hizo, hakimu Mujaya alisema hata naye ameshangaa na kuagiza upande wa mashtaka kulifuatilia jalada hilo ikiwamo kimwandikia mpelelezi wa kesi hiyo ili aweze kuwajibu. Kesi imeahirishwa hadi Aprili 16, 2019 itakapotajwa.

 



Chanzo: mwananchi.co.tz