Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jalada kesi ya vigogo wa TPA latua kwa DPP

Upelelezi Pic DPP VIGOGO Jalada kesi ya vigogo wa TPA latua kwa DPP

Wed, 8 Feb 2023 Chanzo: mwanachidigital

Upande wa mashtaka katika kesi inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA), Madeni Kipande (66) na wenzake watano umedai kuwa jalada la shauri hilo lipo kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) kwa ajili ya uamuzi.

Kipande na wenzake wanakabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Sh4.2 bilioni.

Wakili wa upande wa mashtaka, Mosie Kaima alieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kubwa shauri hilo lilikuja kwa ajili ya kutajwa na upelelezi unaendelea.

Kaima alidai jalada la shauri hilo lipo Dodoma kwa DPP linafanyiwa kazi kwa ajili ya uamuzi, hivyo aliiomba mahakama hiyo iharishe shauri hilo.

Wakili wa utetezi, Omary Msemo aliwataka upande wa mashtaka kuhakikisha wanalifanyia haraka ili kesi iweze kufika mwisho.

Hakimu Mwandamizi, Ramadhan Rugemarila ameahirisha shauri hilo hadi Machi 3, 2023 kwa ajili ya kutajwa tena.

Mbali na Kipande, washtakiwa wengine ni Peter Gawile (58), Ofisa Rasilimali Watu wa TPA, Casmily Lujegi (65), Mwenyekiti wa Bodi ya Manunuzi wa TPA, Mashaka Kisanta (59), Mkurugenzi wa Idara ya Manunuzi na Kilian Chale (51), Kaimu Mkurugenzi Idara ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.

Katika kesi ya msingi, inadaiwa kati ya Oktoba Mosi, 2014 na Oktoba Mosi, 2020 maeneo ya TPA na maeneo mengine ya Dar es Salaam, washitakiwa kwa makusudi walitangaza zabuni ya Enterprises Planning Resources (ERP).

Inadaiwa walitangaza zabuni hiyo, bila kupata kibali cha bodi ya zabuni ya mamlaka hiyo na kushindwa kufuata kanuni za zabuni, hivyo kutoa malipo ya awali ya asilimia 40 bila idhini ya bodi hiyo, jambo lililoisababisha TPA hasara ya Dola za Marekani 1.8 milioni, sawa na zaidi ya Sh4.2 bilioni.

Chanzo: mwanachidigital