Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jalada kesi ya vigogo wa Nida lapelekwa Mahakama Kuu

80242 Pic+maimu

Wed, 16 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam.  Jalada la kesi inayomkabili  aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) nchini Tanzania, Dickson Maimu na wenzake wanne limepelekwa Mahakama Kuu.

Hayo yameelezwa leo Jumanne Oktoba 15, 2019 na Wakili wa Serikali, Elia Athanas mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Salum Ally.

Athanas amesema jalada hilo limepelekwa Mahakama Kuu ya Tanzania kwa sababu lilikuwa ni moja  baina ya mshtakiwa, Astery Ndege aliyeingia makubaliano na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) na aliachiwa huru baada ya kukiri.

"Hili jalada siyo la kwanza kurudishwa mahakama kuu, majalada yote ya watu waliokiri yamepelekwa Mahakama Kuu," amedai Athanas

Hata hivyo, Wakili wa Utetezi, Semi Malimi aliomba ahirisho fupi.

Kwa upande wake, Hakimu Ally Salum ameahirisha shauri hilo hadi Oktoba 28, 2019.

Pia Soma

Advertisement

Mbali na Maimu washtakiwa wengine  ni Meneja Biashara wa Nida, Aveln Momburi, Ofisa Usafirishaji, George Ntalima, Mkurugenzi wa Sheria, Sabina Raymond na Xavery Kayombo.

Miongoni mwa mashtaka yanayomkabili Maimu na wenzake wanne waliobakia wanaokabiliwa na kesi hiyo ni kuisababishia Serikali hasara ya Sh1.175 bilioni.

Utakatishaji fedha, kughushi, kuwasilisha nyaraka za uongo ili kumdanganya mwajiri wao  na kuisababishia mamlaka hiyo hasara, kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu na matumizi mabaya ya madaraka.

Chanzo: mwananchi.co.tz