Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jalada kesi ya mauaji ya mwanaharakati ‘lasota’ kwa DPP

Sun, 26 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Jalada la kesi ya mauaji ya mwanaharakati wa kupinga ujangili na biashara haramu ya meno ya tembo, Wayne Lotter inayowakabili washtakiwa 17, wakiwemo raia wawili wa Burundi lipo kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) kwa ajili ya kupitiwa.

Wakili wa Serikali, Syliva Mitanto ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Ijumaa Mei 24, 2019 wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa.

Mitanto amedai mbele ya hakimu mfawidhi, Kelvin Mhina kuwa wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa na kutokana na hali hiyo, wanaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Baada ya kusikiliza hoja hizo hakimu huyo aliahirisha kesi hiyo hadi Juni 5, 2019.

Washtakiwa hao wanaotetewa na mawakili Benedict Ishabakaki na Mluge Fabian wanakabiliwa na mashtaka mawili likiwemo la mauaji.

Washtakiwa katika kesi hiyo ya mauaji Namba 19/2017 ni raia wawili wa  Burundi; Nduimana Jonas (40) na Bonimana Nyandwi.

Pia Soma

Wengine ni Godfrey Salamba (42) mkazi wa Kinondoni Msisiri A; Innocent Kimaro (23) mkazi wa Temeke Mikoroshini; Chambie Ally (32) mkazi wa Kia/Boma na ofisa wa benki ya NBC, Robert Mwaipyana (31) mkazi wa Temeke Mikoroshini.

Washtakiwa wengine ni meneja wa Benki ya Backlays, Khalid Mwinyi (33) mkazi wa Mikocheni B; Rahma Almas (37) mkazi wa Mbagala B;  Mohammed Maganga (61) ambaye ni mchimba makaburi;  Allan Mafue, Ismail Mohammed, Leornad Makoye, Amino Sham, Ayoub Selemani, Joseph Lukoa, Gaudence Matemu na Abuu Mkingie.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka,  katika shtaka la kwanza, washtakiwa kwa pamoja wanadaiwa kuwa kati ya Julai Mosi na Agosti 16, 2017 walikula njama ya kufanya mauaji ya Lotter.

Katika shtaka la pili, washtakiwa hao wanadaiwa Agosti 16, 2017 katika makutano ya barabara za Chole na Haile Selasie iliyopo Wilaya ya Kinondoni , wanadaiwa kumuua  Lotter.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz