Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jalada kesi ya mauaji ya mwanaharakati Wayne Lotter, lipo kwa DPP

64385 Pic+mauaji

Thu, 27 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam nchini Tanzania  imeelezwa kuwa jalada la kesi ya  mauaji ya mwanaharakati wa kupambana na ujangili, Wayne Lotter (52), inayowakabili mashtakiwa 17, wakiwemo raia wawili wa Burundi, limerudishwa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) kwa ajili ya kupitiwa.

Jalada hilo ambalo lilikuwa Polisi, limerudishwa kwa DPP kwa ajili ya kupitiwa na kutolewa maamuzi.

Wakili wa Serikali, Wankyo Simon, ameieleza mahakama hiyo, leo Jumatano Juni 26, 2019, wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa.

Simon ameeleza hayo, mbele ya hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Kevin Mhina, wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa.

"Upelelezi wa kesi hii bado haujakamilika na jalada la kesi hii limerudishwa kwa  mkurugenzi wa mashtaka nchini kwa ajili ya kulipitia na kulitolea uamuzi, hivyo tunaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa" amedai Simon

Hakimu Mhina baada ya kusikiliza maelezo hayo aliutaka upande wa mashtaka kuhakikisha kuwa wanafuatilia jalada hilo ili kujua limefikia hatua gani

Pia Soma

Mhina baada ya kueleza hayo, ameahirisha kesi hiyo hadi, Julai 8, 2019 itakapotajwa na washtakiwa wamerudishwa rumande kutokana kesi ya mauaji inayowakabili kutokuwa na dhamana.

Washtakiwa kwa pamoja, wanaokabiliwa na mashtaka mawili likiwemo la mauaji katika kesi ya mauaji namba 19/2017.

Washtakiwa katika kesi hiyo ni raia wawili wa  Burundi, ambao ni Nduimana Jonas(40) maarufu Mchungaji na bonimana Nyandwi.

 

Wengine ni Godfrey Salamba (42) mkazi wa Kinondoni Msisiri A, Inocent Kimaro (23) mkazi wa Temeke Mikoroshini, Chambie Ally (32) mkazi wa Kia/Boma na Ofisa wa benki ya NBC, Robert Mwaipyana (31) mkazi wa Temeke Mikoroshini.

Pia, washtakiwa wengine ni Meneja wa Benki ya Backlays, Khalid Mwinyi (33) mkazi wa Mikocheni B; Rahma Almas (37) mkazi wa Mbagala B;  Mohammed Maganga (61) ambaye ni mchimba makaburi;  Allan Mafue, Ismail Mohammed, Leornad Makoye, Amino Sham, Ayoub Selemani, Joseph Lukoa, Gaudence Matemu na Abuu Mkingie.

Katika kesi ya msingi, washtakiwa kwa pamoja wanadaiwa kati ya Julai Mosi na Agosti 16, 2017 walikula njama ya kufanya mauaji ya Mkurugenzi na Mwanzilishi-Mwenza wa Shirika lisilo la kiserikali la PALMS Foundation, Wayne Lotter (52).

Katika shtaka la pili, washtakiwa hao wanadaiwa Agosti 16, 2017 katika makutano ya barabara za Chole na Haile Selasie iliyopo wilaya ya Kinondoni , wanadaiwa kumuua  Lotter, ambaye  alikuwa mwanaharakati wa kupambana na mauaji ya Tembo.

Chanzo: mwananchi.co.tz