Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jalada kesi ya kusafirisha mirungi larudishwa DCEA

Mizani Ya Haki Jalada kesi ya kusafirisha mirungi larudishwa DCEA

Mon, 3 Jul 2023 Chanzo: Mwananchi

Upande wa mashtaka katika kesi inayomkabili Rhoda Salum umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa jalada limerushwa katika Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) kwa ajili ya upelelezi zaidi.

Mshtakiwa huyo anakabiliwa na kosa la kusafirisha dawa za kulevya aina ya Mirungi zenye uzito wa kilo 23.84.

Wakili wa Serikali, Eva Kasa amedai hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Richard Kabate leo Julai 3, 2023 wakati shauri hilo lilipokuja kwa ajili ya kutajwa.

Kasa alidai jalada limerudishwa DCEA kwa ajili ya upelelezi hivyo wanasubiri maelekezo kutoka ofisi hiyo.

"Jarada limerudishwa tena DCEA kwa ajili ya upelelezi zaidi na tunaomba tarehe nyingine ya kutajwa," amedai Kasa.

Hakimu Kabate baada ya kusikiliza hayo ameahirisha kesi hiyo hadi Julai 17, 2023 itakapoitwa kwa ajili ya kutajwa.

Katika kesi ya msingi inadaiwa kuwa mshtakiwa huyo alifanya kosa hilo Januari 26, 2023 katika Mtaa wa Wailes, Wilaya ya Temeke.

Inadaiwa kuwa siku ya tukio mshtakiwa alikutwa akisafirisha kilo 23.84 za dawa za kulevya aina ya mirungi kinyume na sheria.

Chanzo: Mwananchi