Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jalada kesi ya dawa za kulevya inayomkabili mume na mkewe mikononi mwa DCEA

Sat, 27 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es salaam. Jalada la kesi ya kukutwa na dawa za kulevya inayomkabili Ayub Mfaume Kiboko na mkewe, Pilly Mohamed Kiboko lipo katika ofisi za Mamlaka ya Dawa za  Kulevya (DCEA) kwa ajili ya kuchapwa.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Patrick Mwita jana aliieleza hayo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakati shauri hilo lilipotajwa.

Mwita alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Thomas Simba kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika na kwamba wanaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kuangalia kama  utakuwa umekamilika.

"Jalada la kesi hii lipo katika ofisi za Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) kwa ajili ya kuchapwa, hivyo tunaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa, "alisema.

Hakimu Simba baada ya kusikiliza maelezo ya upande wa mashtaka aliahirisha kesi hiyo hadi Novemba 5 itakapotajwa.

Kiboko na mkewe katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 29/2018, wanadaiwa kusafirisha dawa za ku?evya aina ya heroin zenye uzito wa gramu 251.25.

Washtakiwa hao wanadaiwa kuwa Mei 23 eneo la Tegeta Nyuki Masaiti wilaya ya Kinondoni walisafirisha kiasi hicho cha dawa za ku?evya.

Baada ya kusomewa shtaka hilo washtakiwa hawakuruhusiwa kuongea chochote kwa sababu Mahakama ya Kisutu haina mamlaka ya kusikiza kesi hiyo hadi Mahakama Kuu.

Chanzo: mwananchi.co.tz