Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jalada kesi ya bomba la mafuta lipo idara ya upelelezi

9635 Pic+bomba TanzaniaWeb

Thu, 2 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar Es Salaam. Jalada halisi la kesi ya Uhujumu Uchumi inayomkabili mfanyakazi mstaafu wa Shirika la Mafuta Tanzania na Zambia (Tazama), Samwel Nyakirang'ani (63) na wenzake, limepelekwa Polisi, Idara ya Upelelezi  kwa ajili ya kuchapwa.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Patrick Mwita amesema hayo leo Agosti Mosi  mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa  mahakama hiyo, Thomas Simba, wakati shauri hilo lilipokuja kwa ajili ya kutajwa.

Mwita amedai kuwa baada ya kumalizika kuchapwa kwa jalada hilo, litapelekwa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) kwa ajili ya kulitolea maamuzi.

"Kesi ilikuja kwa ajili ya kutajwa na upelelezi wa shauri hili bado haujakamilika na kwamba jalada la kesi hii limerudishwa polisi, Idara ya Upelelezi  kwa ajili ya kuchapwa na baada ya kuchapwa litapelekwa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) kwa ajili kulifanyia maamuzi " amedai Mwita.

Wakili wa utetezi, Alex Balomi aliomba upande wa mashtaka kuongeza juhudi za kukamilisha upelelezi  kwa haraka kwa sababu wateja wao bado wanaendelea kusota.

“Ni rai yetu upande wa mashtaka waongeze juhudi za kukamilisha upelelezi haraka kwa sababu wateja wetu wanaendelea kusota mahabusu” amedai Balomi.

Baada ya maelezo hayo, Hakimu Mkazi Mkuu anayesikiliza shauri hilo, Thomas  Simba aliutaka upande wa mashtaka kuhakikisha wanakamilisha upelelezi haraka, ili kesi hiyo iweze kuendelea.

 Hakimu Simba, ameahirisha kesi hiyo hadi Agosti 14, mwaka huu itakapotajwa.

Mbali Samweli, washtakiwa wengine katika kesi  hiyo namba 1 ya mwaka 2018, ni Nyangi Mataro( 54) mwalimu wa shule ya  msingi Ufukoni na mkazi wa Kisiwani Mkajuni Kigamboni.

 Mfanyabaishara, Farijia Ahmed(39)mkazi wa Soko Maziwa Kigamboni, Malaki Mathias(39) mkazi wa Magogoni, Kristomsi Angelus(25) mkazi wa Soko Maziwa,  Fundi Ujenzi Pamfili Nkoronko(40) mkazi wa Tungi Kasirati na Hunry Fredrick (38) mkazi wa Tungi Kigamboni na Audai Ismail (43) ambaye ni mkazi wa Kibaha, mkoani Pwani

Kwa pamoja washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka matatu ya uhujumu uchumi kwa kujiunganishia isivyo halali bomba la mafuta ya dizeli, kinyume cha sheria  ya uhujumu uchumi.

Chanzo: mwananchi.co.tz