Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jalada kesi ya akina Ringo Tenga lasota kwa DPP

9977 Tenga+pic TanzaniaWeb

Sat, 4 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Jalada la kesi ya  uhujumu uchumi inayowakabili vigogo wanne wa Kampuni ya Six Telecoms, akiwemo Dk Ringo Tenga, bado lipo kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), kwa ajili ya kulipitia.

Lipo kwa DPP baada ya kukamilika kwa  upelelezi pamoja na kufanyika kwa taratibu nyingine za uchapaji wa maelezo na vielelezo vya mashahidi.

Hayo yameelezwa leo Ijumaa Agosti 3, 2018 na wakili wa Serikali, Jacquline Nyatore katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakati shauri hilo lilipofikishwa kwa ajili ya kutajwa.

Nyantore amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa jalada la  shauri hilo bado linaendelea kupitiwa na DPP kwa ajili ya kulitolea maamuzi.

Soma Zaidi:

Jalada kesi ya akina Tenga lipo kwa DPP

Awali, wakili wa utetezi, Bryson Shayo ameutaka upande wa mashtaka kuhakikisha unazingatia tarehe inayopangwa na mahakama.

Ametaka siku hiyo upande huo wa mashtaka kuja wakiwa wamekamilisha kwa maelezo kuwa tangu Februari 2018, ilielezwa kuwa upelelezi umekamilika.

Baada ya maelezo hayo, Hakimu Simba ameutaka upande wa mashtaka kuhakikisha tarehe hiyo, ushahidi uwe umekamilishwa ili kesi iwezi kuanza.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti17, 2018 itakapotajwa tena huku washtakiwa wakirejeshwa rumande kutokana na mashtaka yanayowakabili kutokuwa na dhamana.

Mbali na Dk Tenga, washtakiwa wengine ni mhandisi Hafidhi Shamte au Rashid Shamte ambayeni mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo, mfanyabiashara na mkurugenzi wa kampuni hiyo, Peter Noni na mkuu wa fedha wa kampuni hiyo, Noel Chacha na Kampuni ya Six Telecoms.

Dk Tenga ambaye ni mkurugenzi na mwanasheria wa kampuni hiyo na wenzake wanakabiliwa na mashtaka sita yakiwemo ya utakatishaji wa fedha ambayo hayana dhamana kwa mujibu wa sheria

Chanzo: mwananchi.co.tz