Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jaji kesi ya kina Mbowe kutoa uamuzi kupokelewa hati ya ukamataji

Kesi Mbowe 2 Pic Jaji kesi ya kina Mbowe kutoa uamuzi kupokelewa hati ya ukamataji

Tue, 9 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Leo Jumanne Novemba 9, 2021 Jaji Joachim Tiganga anatarajia kutoa uamuzi kuhusiana hati ya ukamataji mali iliyopingwa na mawakili wa upande wa utetezi kesi ya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu.

Hiyo ni baada ya jana Jaji Tiganga anayesikiliza kesi hiyo kuiahirisha kutokana na mvutano wa mawakili wa pande mbili baada ya mawakili wa utetezi kupinga mahakama hiyo kuipokea hati ya ukamataji mali za washtakiwa wawili katika kesi hiyo.

Mvutano huo uliibuka waakati upende wa mashtaka ulipoiomba Mahakama ipokee hati hiyo kupitia shahidi wa nane, Mrakibu wa Polisi Jumanne Malangahe, wakati akitoa ushahidi wake

Chanzo: www.tanzaniaweb.live