Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jaji Kileo apanda kizimbani kutoa ushahidi kesi ya mauaji

44169 Kileo+pic Jaji Kileo apanda kizimbani kutoa ushahidi kesi ya mauaji

Thu, 28 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Hatimaye Mahakama Kuu imepokea ushahidi wa kesi ya mauaji ya mfanyakazi wa ndani wa kike aliyekuwa akifanya kazi kwa Jaji mstaafu, Engera Kileo anayedaiwa kuuawa na mfanyakazi mwenzake wa ndani wa kiume.

Jaji Kileo ambaye ni mstaafu wa Mahakama ya Rufani ni miongoni mwa mashahidi wa upande wa mashtaka wanaotoa ushahidi katika kesi hiyo akiwa ndiye shahidi wa kwanza.

Akitoa ushahidi wake, Jaji Kileo aliieleza Mahakama alivyopata taarifa za mauaji hayo na jinsi mshtakiwa alivyokuwa akidai kuwa mshtakiwa alikiri mbele yake kufanya mauaji, hivyo akamtaka aweke sawa mambo yake na Mungu.

Katika kesi hiyo ya jinai namba 96 ya mwaka 2016, mshtakiwa Philemon Laizer anadaiwa kumuua Lucy Maina kwa kukusudia. Philemon mwenyeji wa Arusha na Lucy ambaye alikuwa raia wa Kenya, wote walikuwa wafanyakazi nyumbani kwa Jaji Kileo.

Philemon anadaiwa kumuua Lucy Juni 8, mwaka 2013, usiku wa manane nje kidogo ya nyumba hiyo eneo la nyumba za viongozi wa Serikali Mikocheni B, ikidaiwa ni sababu za kimapenzi na kumtupa kwenye dampo kichakani.

Kesi hiyo ilianza kusikilizwa juzi na Jaji Yose Mlyambina, baada ya kimya cha takribani miaka sita.



Chanzo: mwananchi.co.tz