Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Isome hapa hukumu ya kesi iliyoendeshwa miaka 10

Hukumu Pc Data Isome hapa hukumu ya kesi iliyoendeshwa miaka 10

Fri, 19 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Rufani imetoa hati ya kuwakamata na kuwaweka rumande washtakiwa wanne, akiwamo aliyekuwa mfanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Idara ya Wafanyabiashara Wakubwa, Justice Katiti.

Awali, wajibu rufani walishtakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu katika kesi ya Jinai namba 152 ya mwaka 2010 kwa mashtaka kumi, yakiwamo kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu.

Washtakiwa hao wanadaiwa kula njama, kufanya uhalifu, kughushi, kuwasilisha nyaraka za kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu Sh338 milioni na kutakatishaji fedha haramu.

Mahakama hiyo imewatia hatiani washtakiwa hao, baada ya kutengua uamuzi wa hukumu iliyotolewa na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ya kuwaachia huru washtakiwa hao, baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka dhidi ya mashtaka hayo.

Mbali na Katiti, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ya rufaa namba 15/2018 ni Robert Mbetwa na Gidion Otullo, waliokuwa wafanyabiashara na Godwin Paula aliyekuwa mfanyakazi wa Benki ya Barclays.

Uamuzi huo ulitolewa na jopo la majaji watatu wa Mahakama hiyo, wakiongozwa na Shaban Lila, Ignas Kitusi na Liliani Mashaka, wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya kutolewa uamuzi.

Katika uamuzi huo, jopo hilo la majaji limeamuru wajibu rufani wawekwe mahabusu huku jalada la kesi hiyo, likielezwa kurejeshwa Mahakama Kuu kwa ajili ya kutoa adhabu.

Awali, jopo la mawakili watatu waandamizi, likiongozwa na Nassoro Katuga, Hellen Moshi na Tumaini Mafuru, walidai Serikali ilikata rufaa baada ya kutoridhika na hukumu iliyotolewa Mahakama ya Kisutu na Mahakama Kuu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live