Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

"Internet" yakwamisha kesi ya Mbowe Kisutu

MBOWE MTANDAO Freeman Aikael Mbowe

Thu, 5 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkuu Thomas Simba, imeihairisha kesi ya Ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Freeman Aikael Mbowe, hadi kesho Agosti 2 mwaka huu kutokana na hitilafu ya kimtandao iliyojitokea.

Kiongozi huyo atalazimika kufikishwa Mahakamani hapo siku ya kesho kwa ajili ya usikilizwaji wa kesi hiyo.

Taarifa zinaeleza kuwa Mahakama iliamua kutumia mfumo huo wa video kusikiliza kesi hii ili kupunguza msongamano Mahakamani hapo kama njia ya kujikinga na maambukizi ya Covid-19.

Mawakili wa utetezi hadi sasa wapo 470 wakiongozwa na WakiliPeter Kibatala, hata hivyo wananchama wa chama hicho wamejitokeza Mahakamani huku wakiwa na mabango yaliyosomeka "Mbowe sio Gaidi".

Chanzo: www.tanzaniaweb.live