Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Inasikitisha! Mtoto aliyebakwa na kuuawa, baba asimulia mazito

Baka Ml Mtoto aliyebakwa na kuuawa, baba asimulia mazito

Fri, 3 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtoto Rachel Michale Mayala mwenye umri wa miaka 7 ameuawa kikatili kwa kuzibwa mdomo na chandarua wakati akibakwa na kijana ambaye amefahamika kwa jina la Ngosha

Kijana huyo anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka (40) alimfanyia kitendo hicho cha unyama mwanafunzi huyo wa darasa la pili Shule ya Msingi Misugusugu.

Akizungumza kwa huzuni kuhusu tukio hilo, baba mzazi wa marehemu, Michale Mayala maarufu kama Makelele Kulwa nyumbani kwake Kwembe Ubungo Dar es Salaam, amesema Rachel alikuwa mtoto wake wa tatu. Alikuwa akiishi na mama yake baada ya wanandoa hao kutengana.

"Siku ya tukio mtoto aliondoka asubuhi kwenda shule, akiwa na mwenzake akafika sehemu kuna mjomba wake (si wa kuzaliwa na mama yake) wanafahamiana tu kwani amewahi kuishi na mama yake, akasema apite kumsalimia kwani alishazoea huwa anapita mara kwa mara.

"Alipongia pale ndani hakutoka, mwenzake akasubiri mpaka akachoka, akaamua kwenda shule. Rachel hakwenda shule, hata muda wa kurudi nyumbani ulipofika mtoto hakuonekana, ndipo mama yake akapatwa wasiwasi alipowauliza wanafunzi wenzake wakasema hakuwepo shule siku hiyo.

"Zikaanza jitihada za kumtafuta, ambapo mpaka usiku saa 2 ndipo Rachel alipokuwa akiwa amebakwa na kunyongwa kwenye chumba cha huyo kijana anaitwa Ngosha,” amesema Mzee Mayala.

Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, ACP Pius Lutumo imesema kuwa, mtuhumiwa alitendea tukio hilo nyumbani kwake.

Amesema kuwa, tukio hilo limetokea Mei 30,mwaka huu huko mtaa wa Vitendo Misugusugu Kata ya Misugusugu wilayani Kibaha ambapo baada ya tukio hilo mtuhumiwa huyo alitoroka.

Lutumo amesema kuwa, uchunguzi wa awali umebaini kuwa mtuhumiwa alifanya tukio hilo la mauaji wakati akimbaka mwanafunzi huyo ambapo aliziba mdomo kwa kutumia chandarua ili asipige kelele na kusababisha kifo hicho.

Aidha, amesema kuwa wazazi na walezi wanapaswa kuwafuatilia watoto wao na kuzungumza nao mara kwa mara juu ya kujilinda wenyewe kwa kutoa taarifa za haraka juu ya wanaowasumbua.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live