Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ilipofikia kesi ya Seth wa IPTL "DPP mpya anasubiriwa"

Screenshot 2021 06 04 At 09.59.44 660x400.png Ilipofikia kesi ya Seth wa IPTL "DPP mpya anasubiriwa"

Fri, 4 Jun 2021 Chanzo: millardayo.com

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisuru imeelezwa kuwa, mazungumzo ya makubaliano (Plea bargaining) ya kumaliza kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mkurugenzi wa Kampuni ya Kufua Umeme (IPTL), Herbinder Seth yanasuburi Muongozo wa Mkurugenzi mpya wa Mashtaka (DPP).

Wakili wa serikali Mwandamizi Wankyo Simon ameeleza hayo leo Juni 3, 2021 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa na kujua hatma ya mazungumzo hayo na upelelezi ulipofikia.

“Mheshimwa Hakimu, kesi leo imekuja kwa ajili ya kutajwa, upelelezi bado na pia mazunguzo ya kumaliza kesi dhidi ya mshtakiwa Seth yanaendelea pale yalipoishia, tunasuburi muongozo kutoka kwa DPP mpya aliyeteuliwa hivi karibuni na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ili tuweze kuwakilisha hapa mahakamani.

Chanzo: millardayo.com