Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

#IRINGA: Atiwa mbaroni kwa kulawiti kijana miaka 14

#IRINGA: Atiwa Mbaroni Kwa Kulawiti Kijana Miaka 14 #IRINGA: Atiwa mbaroni kwa kulawiti kijana miaka 14

Thu, 13 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Mkoani Iringa limemkamata Blass Nicholous (35) maarufu kama Matowa ambaye ni Mkazi wa Kitasengwa Kata ya Isakalilo katika Manispaa na Mkoa wa Iringa akituhumiwa kumlawiti Kijana wa kiume mwenye umri wa miaka 14 aliyehitimu elimu ya msingi Wilayani Mufindi mwaka 2023.

Kaimu RPC wa Iringa, Alfred Mbena amesema;

“Mtuhumiwa huyo ambaye alikuwa ni Mwajiri wa Kijana huyo ametenda kosa hilo nyumbani kwake Kitasengwa wakiwa wamelala June 09, 2024 majira ya saa 5 usiku huko Kitasengwa Kata ya Isakalilo Manispaa ya Iringa ambapo Kijana huyo alirudi nyumbani kutoka dukani anapouza duka la Mwajiri wake ambaye sasa ni Mtuhumiwa na kwenda kulala pamoja katika chumba wanacholala siku zote tangu alipomwajiri kuuza duka hilo.

“Baada ya kupanda kitandani na kulala muda mfupi Mtoto alisikia mtuhumiwa Blass Matowo ambaye ni Boss wake akimuita akafungue mlango ndipo alipoamka na kwenda kufungua na kurudi kulala, akiwa amelala kitandani alimuona Mtuhumwa anavua nguo zote na kupanda kitandani na kisha kujifunika pamoja nae, wakiwa wamelala pamoja, Mtuhumiwa Blass alianza kumvua suruali mhanga na kumuingizia uume sehemu ya haja kubwa ambapo mhanga alihisi maumivu makali ndipo alipoamka na kwenda kulala sebuleni kwenye kochi”.

“Hata hivyo asubuhi ya June 10, 2024 Mhanga alianza kuhisi maumivu ya tumbo na alipomaliza kuoga alijiandaa na kwenda dukani kwa Boss wake kuendelea na kazi, akiwa dukani alikuja mama yake mlezi (Mama P) na kumueleza kuwa Matowo amemfanyia kitendo hicho kibaya na kisha Mama huyo Mlezi alienda kumueleza Mume wake ambaye ni Rafiki wa Mtuhumiww huyo na ndipo alipowashirikisha pia Viongozi wa Mtaa kwa hatua zaidi”

“Mtuhumiwa baada ya kuhojiwa amekana kuwa hajafanya kitendo hicho ambapo pia uchunguzi unaendelea na pindi uchunguzi ukibainika atafikishwa Mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live