Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

IGP: Wahujumu SGR wakamatwe

Ea3f9bacda6c4f6e887855ef75b3e2ed IGP: Wahujumu SGR wakamatwe

Sat, 28 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MKUU wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP), Simon Sirro amewaagiza makamanda wa Polisi kwenye mikoa wafanye ukaguzi kwenye maeneo wanakokukusanya na kuuza vyuma chakavu ili kubaini watu wanaohujumu miundombinu ya ujenzi wa Reli ya Kisasa ya (SGR).

IGP Sirro alitoa kauli hiyo kwenye Kituo cha Polisi kiwilaya Mlandizi, Kibaha baada ya Polisi kukamata gari lililokutwa na vyuma vilivyoibwa kwenye miundombinu ya SGR.

Alisema Polisi wanapaswa kuvichunguza vyuma hivyo kwa kuwa watu wanaofanya uhalifu huo wanahujumu uchumi wa nchi.

“Watanzania wanapaswa kuachana na tabia ya kujihusisha na tabia za kuchukua vyuma vya reli, wanahujumu nchi na watakuwa wamejiingiza kwenye matatizo makubwa,” alisema IGP Sirro.

Aliwapongeza askari kwa kulikamata gari hilo aina Mitsubishi Fuso lenye namba za usajili T 167 DJW likiwa limebeba vyuma chakavu vilivyokuwa vimechanganywa na vyuma vya reli hiyo ya kisasa.

“Watanzania wanapaswa kuheshimu miundombinu hii kwa faida yetu wenyewe na watu waachane na vitendo hivi vya kuhujumu miundombinu hii muhimu kwa uchumi na maendeleo ya Taifa,” alisema Mkuu wa Polisi nchini.

Aliutaka uongozi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) utoe elimu kwa kwa aksari wa Jeshi la Polisi ili iwe rahisi kwao kufahamu vifaa vinavyotokana na miradi ya reli kurahisisha udhibiti wa wizi kama huo.

Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Masanja Kadogosa alisema kuna madhara makubwa kwa watu wanaohujumu miundombinu hiyo, na kubainisha kwamba wamekuwa wakishirikiana na Polisi kudhibiti wizi unaofanyika kwenye mradi huo na miradi mingine inayotekelezwa na shirika hilo.

Chanzo: habarileo.co.tz