Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

IGP Sirro kuchunguza alipo mbwa wa Bandari

11888 Sirro+pic TanzaniaWeb

Sun, 22 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Waziri wa Mambo ya Ndani,  Kangi Lugola amesema Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP),  Simon Sirro anaendelea kuchunguza kwa undani alipo mbwa maalum wa polisi kikosi cha Bandari ambaye hajulikani alipo.

Mbali na mbwa huyo, amesema wengine 30 waliokuwa wakiondolewa na kurejeshwa kinyemela pia wanachunguzwa.

Lugola ametoa kauli hiyo leo Jumamosi Julai 21, 2O18 wakati akitoa taarifa ya ziara aliyoifanya mkoani hapa kuanzia Julai 11, 2O18.

"Nimemuagiza Sirro kuchunguza kwa undani na kubaini nini kimetokea kisha  kuniletea taarifa. Wafanye uchunguzi kiundani zaidi kubaini nini kimetokea kwenye kikosi hicho na kunipa taarifa,” amesema Lugola.

Julai 19, 2018 Lugola alisema anahitaji maelezo kutoka kwa Sirro kuhusu alipo mbwa huyo huku jana akibainisha kuwa hakuwa amepata maelezo yoyote kuhusu alipo mbwa huyo.

Lugola alitoa kauli hiyo alipofanya ziara Bandari ya Dar es Salaam kwa ajili ya kuona utendaji kazi wa jeshi la polisi bandarini hapo.

Amesema alibaini kati ya mbwa sita maalum, wawili wapo mafunzoni na wanabaki wanne ambapo kati yao mmoja aitwaye Hobby hajulikani alipo tangu Julai 18, 2018.

Amebainisha kuwa kuwa kikosi cha farasi na mbwa kinachosimamia bandarini kinatakiwa kuboreshwa na kuwa katika mazingira salama.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz