Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

IGP Sirro azungumzia mauaji ya raia tisa wa Watanzania

65618 Sirro+pic

Fri, 5 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Inspekta Jenerali wa Polisi nchini Tanzania (IGP), Simon Sirro amesema baadhi ya watu wanaotuhumiwa kuhusika katika mauaji ya Watanzania tisa nchini Msumbiji wamekamatwa.

 

Juni 26 mwaka 2019 watu 11 wakiwemo Watanzania tisa na raia wa Msumbiji waliuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana katika kijiji cha Mtole kinachopakana na kijiji cha Kiamba mkoani Mtwara upande wa Tanzania.

 

Watanzania hao walikwenda katika kijiji hicho kujitafutia riziki ikiwemo kufanya kilimo cha mpunga katika kambi ambazo kila wakati wanakwenda kufanya shughuli hizo

 

Pia Soma

 Jana jioni, IGP Sirro akizungumza na Redio Cloud FM alisema watuhumiwa hao walikamatwa licha ya kutotaja idadi yao.

 

“Kuna baadhi ya watu wamekamatwa, kati yao mmoja alikimbia kuja maeneo ya Ruvuma (Tanzania), lakini alipigwa risasi. Sasa hivi hali ni shwari na ulinzi tukishirikiana na wenzetu wa Msumbiji,” amesema IGP Sirro.

Chanzo: mwananchi.co.tz