Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

IGP Simon Sirro kazungumzia ugaidi ziarana Rwanda

Sirroo Rwanda56 Ziara ya Kamanda Sirro Nchini Rwanda

Wed, 8 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Simon Sirro, Amewasili nchini Rwanda kwa jili ya ziara ya ya kikazi ya Wakuu wa Jeshi la Polisi, kujadili kuhusu changamoto za uhalifu unaovuka mipaka.

Amepokelewa na Maofisa waandamizi wa Jeshi la Polisi nchini Rwanda wakiongozwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi humo Dan Munyuza.

Kamanda Sirro amesema kuwa wataendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi Rwanda katika kubadilishana taarifa za uhalifu na wahalifu hususani wenye viashiria vya ugaidi ili kuzuia vitendo hivyo kabla havijatokea na kuleta madhara kwa wananchi.

"Hakuna muda wa kujadiliana na gaidi, anapo kamatwa anapaswa awajibishwe, tunapaswa kuhakikisha tunalifanyia kazi suaala hili kwa haraka, ugaidi kwa sasa ni jambo linaloibuka kwa kasi" Kamanda Sirro

Aidha amelitaka Jeshi la Polisi nchini humo kutoa ushirikiano pale watakapo hitaji taarifa zinazo wahalifu aina ya waliowakamata ili kutokomeza matukio ya ugaidi kwa nchi zote mbili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live