Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Huzuni! Mjamzito achomwa kisu mara tano

Kisu Nyetiii.jpeg Huzuni! Mjamzito achomwa kisu mara tano

Fri, 9 Jun 2023 Chanzo: Millard Ayo

Msichana mwenye umri wa miaka 17 ambaye ni mjamzito Mkazi wa Dumila Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro amejeruhiwa kwa kuchomwa kisu mara tano sehemu mbalimbali za mwili wake huku akidai kufanyiwa kitendo hicho na Mzazi mwenzake ambaye alimgomea kwenda kulala nae kwakuwa walishaachana.

Msichana huyo ambaye kwa sasa amelazwa katika Hospitali ya Mtakatifu Joseph Dumila amesema saa saba usiku May 5,2023 wakati akirudi kutoka kwenye sherehe ya Rafiki yake alivamiwa na Mzazi mwenzake kisha kupakiwa kwenye pikipiki kwa nguvu na kuondoka nae na akamjeruhi tumboni, kichwani, mgongoni huku kisu kikivunjikia kwenye paja akimlazimisha waende kulala wote huku akijua wameachana zaidi ya miezi mitatu sasa.

Mganga Mfawidhi Hospitali ya Mtakatifu Joseph, Dokta Manyele Kapongo alikolazwa majeruhi huyo amesema vipimo vya utra sound vimeonesha kisu alichochomwa tumboni hakikufika kwenye utumbo na mfuko wa uzazi haujaathiriwa na jeraha hilo lakini Msichana ana ujauzito wa Wiki saba.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Njia Panda Sadick Kazikula ambako tukio limetokea na ambaye pia ni Shuhuda amethibtisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema wakati tukio linatokea walikua kwenye ulinzi (Sungusungu) na waliposikia kelele baada ya kufika eneo la tukio Mtuhumiwa alikuwa ameshakimbia hivyo walimchukua majeruhi na kumpeleka Hospitali.

Jitihada za kumtafuta RPC Morogoro zinaendelea ili kufahamu hatua ambazo Jeshi hilo limezichukua kutokana na tukio hilo.

Chanzo: Millard Ayo