Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hukumu ya mjane wa Bilionea Msuya yaanza kusomwa

Msuya Msdf Hukumu ya mjane wa Bilionea Msuya yaanza kusomwa

Fri, 23 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imeanza kusoma hukumu ya kesi ya mauaji inayomkabili mjane wa aliyekuwa mfanyabiashara maarufu wa madini jijini Arusha, Erasto Msuya maarufu kama Bilionea Msuya, Miriam Mritabna mwenzake Revocatus Muyella maarufu kwa jina la Ray.

Hukumu hiyo inasomwa leo Ijumaa Februari 23, 2024 na Jaji Edwin Kakolaki aliyeisikiliza.

Washtakiwa hao, Miriam na Muyella wanakabiliwa na shtaka moja la mauaji ya kukusudia la kumuua Aneth Elisaria Msuya (wifi wa Miriam) aliyekuwa mdogo wa Bilionea Msuya.

Aneth aliuawa kwa kuchinjwa na kitu chenye ncha kali nyumbani kwake Kibada Kigamboni, Dar es Salaam Mei 25, 2016.

Katika hukumu hiyo Jaji Kakolaki ameanza kwa kurejea shtaka linalowakabili kisha ushahidi wa upande wa mashtaka akifanya muhtasari wa ushahidi wa kila shahidi.

Kisha atarejea utetezi wa washtakiwa kabla ya kuchanganua namna gani upande wa mashtaka umeweza au umeshindwa kuthibitisha shtaka bila kuacha shaka kwa washtakiwa wote.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live