Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hukumu ya anayedaiwa kumtukana Rais Museveni yaiva

67060 HUKUM+PIC

Wed, 17 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kampala. Mahakama Kuu nchini Uganda imepanga Agosti Mosi, 2019 kutoa hukumu ya mwanaharakati anayedaiwa kumtukana  Rais wa nchi hiyo, Yoweri Museveni.

Hukumu hiyo itatolewa baada ya mahakama hiyo kumkuta mwanaharakati huyo, Dk Stella Nyanzi na kesi ya kujibu.

Dk Nyanzi, mtafiti wa Chuo Kikuu cha Makerere Uganda anadaiwa kumtukana Museveni na familia yake kupitia akaunti yake ya facebook.

Kwa mujibu wa gazeti la The Monitor la nchini Uganda, mahakama hiyo iliyopo katika barabara ya Baganda ilitoa uamuzi wake mara baada ya kusikiliza ushahidi kutoka kwa mashahidi watatu wa Serikali.

Hakimu, Gladys Kamasanyu anayesikiliza kesi hiyo amesema Dk Nyanzi anamiliki akaunti ya Facebook ambao ulichapisha matusi hayo.

Mwanaharakati huyo anashtakiwa kwa kutekeleza unyanyasaji wa mtandaoni pamoja na kutoa matamshi machafu suala ambalo linakiuka sheria za nchi hiyo.

Pia Soma

Mwanaharakati huyo kwa sasa yupo rumande katika gereza la Luzira baada ya kukataa kuomba dhamana.

Awali,  ilidaiwa mahakamani hapo kuwa Septemba 16, 2018,  Dk Nyanzi alichapisha katika ukurasa wake wa Facebook madai hayo kuhusu Museveni.

Pia, Dk Nyanzi anatuhumiwa kuchapisha ujumbe wa kuvuruga amani, utulivu na kuingilia faragha ya Rais Museveni.

Hii ni mara ya pili maofisa wa polisi wanamtuhumu,  Dk Nyanzi kwa madai ya kumtusi Rais Museveni na familia yake.

Chanzo: mwananchi.co.tz