Fri, 6 May 2022
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, leo Mei 6, 2022 inatarajiwa kutoa hukumu ya rufani namba 129, katika Kesi ya Jinai iliyokuwa inamkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wa wawili.
Februari 14, 2022 Mahakama hiyo ilianza kusikiliza hoja 14 za Waleta Rufani kupinga adhabu ya hukumu ya kifungo cha miaka 30 jela iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi, Mkoa wa Arusha.
Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Silvester Nyegu na Daniel Mbura, waliokuwa wakikabiliwa na mashtaka matatu ya unyang'anyi kwa kutumia silaha
Chanzo: www.tanzaniaweb.live