Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hukumu ya Mwijaku kutolewa Mei 31

Mwijaku Pic Data Msanii wa maigizo, Mwemba Burton maarufu kama Mwijaku

Wed, 11 May 2022 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu imepanga Mei 31, 2022 itatoa hukumu ya kesi ya kusambaza picha za utupu inayomkabili msanii wa maigizo, Mwemba Burton maarufu kama Mwijaku.

Hiyo ni baada ya Mwijaku na wenzake wawili kumaliza kutoa ushahidi wao na kisha kufunga ushahidi wa upande wa utetezi leo Jumatano Mei 11, 2022.

Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Rhoda Ngimilanga amepanga tarehe hiyo baada ya mashahidi hao wa upande wa utetezi kumaliza kutoa ushahidi wao.

"Nitatoa hukumu Mei 31, 2022 na mshtakiwa utaendelea kuwa nje kwa dhamana" amesema Hakimu Ngimilanga.

Mwinjaku alikutwa na kesi ya kujibu wiki iliyopita baada ya mahakama kupitia ushahidi wa mashahidi watano na vielelezo vinne vilivyotolewa na upande wa mashtaka.

Awali, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mwanaamina Kombakono aliieleza mahakama hiyo, kuwa shauri hilo limeitwa kwa ajili ya Mwijaku kuanza kujitetea na upande wa mashataka upo tayari.

Hata hivyo, Mwijaku na mashahidi wake wawili wametumia siku ya leo kutoa utetezi wao dhidi ya kesi inayomkabili.

Katika kesi ya msingi, Mwijaku anakabiliwa na kesi ya jinai namba 110/2020.

Mshtakiwa anadaiwa kutenda kosa hilo, kati ya Septemba 17, 2019 na Oktoba 2019 katika Jiji la Dar es Salaam.

Katika kipindi hicho, Mwijaku anadaiwa kuchapishwa picha za ngono kupitia mtandao wa kijamii wa WhatsApp uliunganishwa katika Kompyuta.

Mshtakiwa huyo anadaiwa kusambaza picha hizo, wakati akijua kuwa kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.

Kwa mara ya kwanza, Mwijaku ambaye ni Mkazi wa Mbezi Beach, alifikishwa mahakamani hapo Julai 29, 2020 na kusomewa shtaka hilo.

Chanzo: www.mwananchi.co.tz