Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hukumu ya Malinzi Novemba 7

81730 Pic+malinzi Hukumu ya Malinzi Novemba 7

Fri, 25 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Novemba 7 mwaka huu itatoa hukumu dhidi ya kesi inayomkabili, aliyekuwa rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Jamal Malinzi (57) na wenzake wa wanne. Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi aliyaeleza hayo Oktoba 25, mwaka wakati kesi hiyo ilipokuwa imepangiwa tarehe ya hukumu. Kabla ya Hakimu Shaidi  kueleza hayo, Wakili wa serikali, Ester Martin alieleza kuwa kesi hiyo ilipangwa kwa ajili ya kupangiwa tarehe ya hukumu. Hukumu  hiyo inatarajiwa kutolewa siku hiyo na Hakimu Mkazi, Maira Kasonde ni baada ya kusikiliza ushahidi wa mashahidi 15 wa upande wa mashtaka na kuufunga pamoja na ushahidi wa upande wa utetezi uliotolewa na washtakiwa wenyewe. Washtakiwa katika kesi hiyo mbali na Malinzi, wengine ni Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Joas Selestine (46) na Mhasibu wa TFF,  Nsiande Isawayo Mwanga(27). Wengini ni Meneja wa  Ofisi ya Shirikisho hilo, Miriam Zayumba na Karani wa TFF, Flora Rauya ambao kwa pamoja  wanakabiliwa na mashtaka 30 katika kesi ya jinai namba 213 ya mwaka 2017 yakiwamo ya kula njama, kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji wa fedha wa USD 173,335 na Sh 43,100,000. Malinzi, Mwesigwa na Nsiande wapo rumande kwa kukabiliwa na mashtaka ya utakatishaji fedha kuwa miongoni mwa mashtaka ambayo kwa mujibu wa sheria hayana dhamana huku wenzao Zayumba na Flora wapo nje kwa dhamana.

Chanzo: mwananchi.co.tz