Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hukumu kesi ya wakili Mwale kutolewa Desemba 3

29475 Wakili+pic TanzaniaWeb

Fri, 30 Nov 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arusha. Mahakama Kuu Kanda ya Arusha Jumatatu Desemba 3, 2018 inatarajiwa kusoma hukumu ya kesi inayomkabili wakili maarufu nchini Tanzania, Median Mwale na wenzake wawili baada ya kukiri  makosa.

Katika kesi hiyo wakili Mwale na wenzake, Boniface Mwimbwa aliyekuwa meneja wa Benki ya CRDB tawi la Meru na Elias Ndejembi wanatuhumiwa kwa makosa kadhaa ikiwemo kughushi na utakatishaji fedha.

Hukumu ya shauri hilo inatarajiwa kusomwa na Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Issa Maige.

Katika kesi hiyo, aliyekuwa mshitakiwa wa pili, Donbosco Gichana (raia wa Kenya) alikiri makosa ya kula njama na kutakatisha fedha kiasi cha dola za Marekani  5,296,327.25 na kuamriwa kulipa faini au kutumikia kifungo gerezani.

Gichana alilipa faini hiyo na tayari aliondoka nchini kurejea Kenya.

Mawakili wa Serikali katika kesi hiyo ni  Oswald Tibabyekomya, Hashim Ngole na Pius Hilla huku wale wa upande wa utetezi wakiwa ni Omari  Omari, Emmanuel Mvula na Innocent Mwanga.

Soma zaidi: Wakili Mwale, wenzake wasomewa mashtaka 59



Chanzo: mwananchi.co.tz