Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hukumu kesi ya kugombea mirathi ya bilionea Msuya Januari 28

88432 Billionea+msuya+pic Hukumu kesi ya kugombea mirathi ya bilionea Msuya Januari 28

Sat, 14 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arusha. Wakati Mahakama Kuu Kanda ya Arusha nchini Tanzania, Januari 28, 2019 inatarajiwa kutoa hukumu ya kesi ya kugombea usimamizi wa mirathi ya mali za marehemu, bilionea Erasto Msuya.

Kesi hiyo imefunguliwa na mama mzazi wa  bilionea huyo, Ndeshikurwa Sikawa akitaka mjane wa bilionea huyo, Miriam Mrita kuondolewa kusimamia mirathi.

Kesi hiyo ilitarajiwa kutolewa hukumu leo Ijumaa Desemba 13, 2019 lakini Jaji inayesikiliza kesi hiyo, Yohanes Masara hakuwapo.

Kaimu Naibu Msajili wa Mahakama kuu Kanda ya Arusha, Gwantwa Mwankunga ndiye ameahirisha kesi hiyo.

Katika kesi hiyo namba 66/2019, mama wa bilionea Msuya, anataka mjane wa marehemu Msuya, Miriam Mrita kuondolewa kuwa msimamizi wa mirathi hiyo akimtuhumu kuanza kuuza mali za marehemu mume wake.

Miriam kupitia wakili wake, Shilinde Ngalula aliweka pingamizi juu ya shauri hilo kwa hoja kuwa tayari limetupwa mara mbili na Mahakama Kuu ya Tanzania kutokana na shauri hilo kuwa tayari lilifungwa.

Awali, uamuzi juu ya shauri hilo, ulipangwa Novemba 29, 2019  hata hivyo, Jaji Masara hakuwapo ambapo, Naibu msajili wa Mahakama Kuu, Julius Nkwabi aliahirisha hadi leo Ijumaa Desemba 13, 2019 kwa ajili ya uamuzi.

Wakili Fadhili Nangawe  anayemtetea  mama wa bilionea huyo, aliomba kabla ya hukumu hiyo kutolewa mteja wake aliomba shauri hilo kusitishwa ili wafanye mazungumzo nje ya mahakama.

Akizungumza na Mwananchi, wakili wa mjane wa bilionea Msuya na watoto wake, Shilinde Ngalula alisema katika pingamizi lao, wanapinga kurejesha mahakamani maombi hayo kwani tayari mahakama hiyo ilishafunga jalada la kesi hiyo.

Hata hivyo, alisema walitatajia hadi leo Ijumaa mama wa bilionea Msuya angekuwa amefuta kesi kama ambavyo walikubaliana kwa Mkuu wa wilaya ya Arumeru, Jerry Muro.

"Hadi leo sijapokea taarifa yoyote ya kufutwa kesi hii," amesema

Katika hatua nyingine, kaka Mjane wa bilionea Msuya, Mbazi Mrita alisema mtoto wa bilionea Msuya Glory Msuya aliyekuwa Canada anatarajiwa kufika nchini Januari 18, 2019.

"Tayari tumemtumia tiketi arudi nchini na atakuja kueleza mambo mengi ikiwapo taarifa za kupotoshwa kuwa alikuwa amepotezwa," alisema.

Mtoto wa bilionea huyo, Kelvin Msuya alieleza kushangazwa na bibi yake kukataa kufuta shauri hilo na kuiomba Serikali kuingilia kati ili kesi hiyo imalizike kwa wakati na kesi ya mama yake, ambayo tangu Julai 2019 imesimama.

"Kama tulivyozungumza kwenye ofisi ya mkuu wa wilaya bibi alikuwa aje mahakamani kufuta shauri lakini inasikitisha shauri halijafutwa  hadi leo" alisema.

Mali ambazo zinatajwa katika kesi hiyo  hoteli mbili za kitalii, SG Northern Adventures Limited iliyopo jijini hapa na Mezaluna hoteli iliyopo eneo la kijenge katika jiji la Arusha, nyumba ya makazi iliyopo eneo la kwa Idd wilayani Arumeru na nyumba  ya biashara iliyopo eneo la Kibanda maziwa jijini Arusha.

Mali nyingine zinazogombea ni nyumba ya makazi iliyopo eneo la Njiro PPF, mgodi wa Tanzanite Mererani, Mgodi wa Ruby uliopo lembeni, shamba kubwa lililopo eneo la Ngurudoto wilayani Arumeru.

Nyingine ni pamoja na viwanja vitano  vilivyopo Njiro, kiwanja kilichopo Njiro  nanenane, kiwanja kilichopo eneo la Elboru jijini Arusha,Shamba lililopo eneo la Ikoma Serengeti na nyumba ya ghorofa iliyopo Mererani.

Mali nyingine  ni pamoja na Shamba lililopo wilayani Babati, kiwanja kilichopo eneo la Burka,Magari Range Rover  yenye namba za usajili T800CKF na Range  Rover E- Vogue.

Katika kesi hiyo pia mali ambazo zimetajwa  ni pamoja na gari aina ya Toyota Landcuiser, Ford Rangers yenye namba za usajili T307 CBH, Toyoya Voxy namba T703BRS,Suzuki Escudo na mamilion ya fedha ambayo yanadaiwa yapo benki.

Chanzo: mwananchi.co.tz