Arusha. Hukumu ya kesi inayomkabili mmiliki wa shule ya msingi Lucky Vicent, Innocent Moshi na Mwalimu Mkuu msaidizi katika shule hiyo, Longino Vicent(40) kuhusiana na ajali ya basi la shule hiyo, ambalo liliua wanafunzi 32, walimu mawili na dereva inatarajiwa kusomwa Jumatatu June 10, 2019 baada ya kukamilika uandikaji wa hukumu hiyo .
Ajali hiyo, ilitokea Mei 6, 2017, katika eneo la Rhotia wakati, wanafunzi wa shule hiyo, wakitoka Arusha majira ya saa 12 asubuhi kwenda wilayani Karatu, katika mitihani ya ujirani mwema katika Shule ya Tumaini Academy.
Hakimu mkazi wa mahakama ya mkoa wa Arusha, Niku Mwakatobe ndiye anatarajiwa kusoma hukumu hiyo, baada ya kumaliza kusikiliza mashahidi na mashitaka na utetezi wa watuhumiwa katika kesi ambayo imechukua takriban miaka mitatu sasa na baada ya kumaliza kuandika hukumu.
Hukumu ya kesi hiyo iliyokuwa itolewe leo Ijumaa Juni 7, 2019 imeahirishwa mara tatu, sasa inatarajia kuvutia idadi kubwa ya ndugu, jamaa na marafiki, ambao walipoteza watoto na walimu na dereva katika ajali hiyo.
Katika kesi hiyo, washitakiwa wanakabiliwa na jumla ya mashitaka matano ya kuvunja sheria za usalama barabarani, ikiwepo kuendesha gari za abiria bila kuwa na leseni ya usafirishaji, gari lililosababisha ajali kutokuwa na bima, kushindwa kuingia mkataba baina ya dereva na mwajiri na kosa la kuzidisha abiria 13 katika gari lililopata ajali ambalo linamkabili mwalimu mkuu msaidizi.
Washitakiwa hao, wanatetewa na wakili, Method Kimomogoro ambapo walikana mashitaka hayo, katika utetezi wa mwisho ambao waliutoa Machi 19, 2019.
Pia Soma
- Waziri Mkuu Uingereza May ajiuzulu rasmi wadhifa wake
- VIDEO: Dk Mzindakaya asema Wizara ya Kilimo Tanzania ni mzigo
- VIDEO: Rais Magufuli atamani kuona mabilionea wengi Tanzania
Alisema pia alishitakiwa kwa kosa la kutumia gari bila kuwa na bima na kuwapakia wanafunzi 38 ndani ya basi dogo kinyume na sheria kwani linapaswa kubeba abiria 25
Alisema yeye hajatenda makosa hayo pia kampuni ya Lucky Vicent iliuziwa gari yenye namba T871 BYX na Swalehe kiluvia pamoja na kuwakabidhi kadi ya gari bima ya gari pamoja na leseni ya gari hilo.
Mshitakiwa wa pili Mwalimu Mkuu msaidizi katika shule hiyo, Longino Vicent(40) alieleza mahakama kuwa May 6 waka 2017, alifika shuleni muda wa saa kumi na mbili asubuhi na kushughulikia zoezi la usafiri wa wanafunzi aliopewa na mwalimu mkuu na gari tatu kwenda Karatu.
Vicenti alikanusha kuhusika na ajali hiyo kwani hakuwepo eneo la tukio na yeye alitimiza wajibu wake aliokabidhiwa na mkuu wa shule kuwasafirisha wanafunzi hao wakiwa na walimu wao.