Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hukumu kesi ndogo ya Mbowe imesogezwa mbele

Mpya Mbowe Uamuzi kesi ndogo ya kina Mbowe wapelekwa mbele

Mon, 18 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe na wenzake ya uhujumu uchumi yenye mashtaka ya ugaidi iliyokuwa imepangwa kutolewa uamuzi wa kesi ndogo tarehe 19, 2021 imepelekwa mbele hadi Oktoba 20,2021

Mahakama imefikia hatua hii ili kupisha sikukuu ya Maulid ambayo itafanyika Oktoba 19, 2021.

Inaelezwa kuwa tayari Mkuu wa Mahakama ya Division ya uhujumu uchumi ameshawapatia taarifa rasmi ya wito Mawakili, watuhumiwa pamoja na magereza juu ya mabadiliko hayo ya tarehe.

Kesi hii itaendelea tena tarehe tajwa majira ya saa tatu mbele ya Jaji Christopher Siyani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live