Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hukumu kesi mke wa bilionea Msuya Februari 23

Mke Wa Marehemu Bilionea Erasto Msuya, Miriam Mrita Hukumu kesi mke wa bilionea Msuya Februari 23

Fri, 16 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hukumu ya kesi ya jinai namba 103 ya mwaka 2018, inayomkabili mjane wa aliyekuwa mfanyabiashara wa madini mkoani Arusha, Erasto Msuya maarufu kama Bilionea Msuya, Miriam Steven Mrita na mwenzake Revocatus Muyella imeahirishwa hadi Februari 23, 2024.

Sababu za msingi za kesi hiyo kuahirishwa hazijawekwa wazi isipokuwa mawakili wa pande zote mbili( wa serikali na wa utetezi),walipokea taarifa ya kurudi Februari 23 kwa ajili ya kusomewa hukumu ya kesi hiyo.

Miriam ambae ni mjane wa Bilionea Msuya, aliyeuawa kwa kupigwa risasi eneo la Mijohoroni wilayani Hai mkoani Kilimanjaro, Agosti 7, 2013 na mwenzake Muyella wanakabiliwa na shtaka moja la mauaji, wakidaiwa kumuua Aneth Elisaria Msuya aliekuwa wifi wa Miriam.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live