Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hukumu anayedaiwa kumuua mkewe Jumatatu ijayo

Hukumu Pic G Hukumu anayedaiwa kumuua mkewe Jumatatu ijayo

Tue, 10 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imepanga Januari 16, 2023 kutoa hukumu katika kesi ya mauaji ya kukusudia inayomkabili mfanyabiashara Diblo Said.

Saidi anakabiliwa na shitaka moja la kumuua mke wake aitwaye Herieth Justine kwa kumchoma na kisu tumboni, begani na kifuani, baada ya kumfumania na mwanaume mwingine, tukio analodaiwa kulitenda Machi 11, 2018 katika eneo la Vingunguti.

Mshitakiwa baada ya kumchoma visu mkewe, kisha naye kujichoma kisu mbele ya kituo cha Polisi Vingunguti akiwa na nia ya kujiua baada ya kumfumania mke akiwa na mwanaume mwingine ndani ya nyumba yake.

Kesi hiyo ilipangwa jana Januari 9, 2023 kutolewa hukumu, lakini hakimu Mkazi Mkuu, Evodia Kyaruzi anayesikiliza shauri hilo amesema bado hajamaliza kuandika hukumu na kisha kuahirisha kuahirisha kesi hiyo hadiĀ  Januari 16, 2023 atakaposoma hukumu.

"Hukumu bado sijamaliza kuiandika na kwa bahati mbaya nilikuwa likizo, hivyo kuwa vitu vichache bado sijakamilisha kuviweka katika huku hii, hivyo Diblo nitatoa hukumu yako Jumatatu Janauri 16, 2023," amesema Hakimu Kyaruzi.

Mshtakiwa amerudishwa rumande kutokana na shitaka la mauaji linalomkabili kutokuwa na dhamana kwa mujibu sheria.

Miongoni mwa mashahidi waliowahi kutoa ushahidi dhidi ya mshtakiwa huyo ni Mkaguzi wa Jeshi la Polisi Pudence Emmanuel (47), ambaye alidai kuwa mshtakiwa huyo alivyojipeleka mwenyewe kituo cha Polisi Vingunguti na kisha kujichoma kisu tumboni hadi utumbo ukatoka nje kabla ya kuingia ndani ya kituo hicho.

Emmanuel ambaye kwa sasa yupo ofisi ya Upelelezi na Makosa ya Jinai Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, alidai kuwa Machi 11, 2018, alipokea simu kutoka aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wilaya ya Kipolisi Buguruni, Davis Msangi aende Vingunguti kuna mwanamke mmoja amechomwa kisu kifuani na begani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live