Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Houseboi adaiwa kumnyonga bosi wake hadi kufa

Police Line.jpeg Houseboi adaiwa kumnyonga bosi wake hadi kufa

Thu, 4 Nov 2021 Chanzo: JF

Kijana wa kazi za nyumbani ‘house boy’ (jina tunalihifadhi), anadaiwa kumuua bosi wake kwa kumnyonga kwa kamba ya katani kisha kutokomea.

Tukio hilo lilitokea Jumatatu, Bombani Kata ya Pugu, jijini Dar es Salaam. Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Kamishna Msaidizi wa Polisi Moses Fundi, aliiambia Nipashe jana kwamba mtuhumiwa huyo alimnyonga Cecilia Songomba (56), ambaye alikuwa mkunga mstaafu.

“Inasemekana mtuhumiwa ni mkazi wa Kaliua, mkoani Tabora, walikuwa (familia ya marehemu( wamekaa naye kwa wiki mbili, hiyo nyumba walikuwa wanakaa watu watatu tu, mama (Cecilia), baba ambaye ni mume na huyo kijana,” alisema Kamanda Fundi.

Alisema mume wa Cecilia ambaye wakati wa tukio alikuwa mjini, aliporejea nyumbani aligonga mlango bila kufunguliwa ndipo alipoamua kuruka ukuta ili aingie ndani.

“Alipoona anagonga mlango hafunguliwi, akaona aruke ukuta, aliporuka akakuta huyo mama amenyongwa kwa kufungwa chooni, kwa kamba ya katani.

Kamanda Fundi alisema mtuhumiwa hajakamatwa kwa kuwa baada ya tukio hilo alitoroka.

Chanzo: JF