Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

'House girl' auawa kwa kichapo Moshi

Kifo Kifo Mauiaji.png 'House girl' auawa kwa kichapo Moshi

Fri, 27 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro, linamsaka mkazi wa Kijiji cha Uswaa, wilayani Hai (jina linahifadhiwa kwa sababu za kiuchunguzi), akidaiwa kuhusika kifo cha msichana wake wa kazi 'house girl' ambaye ni mwenyeji wa Mkoa wa Kigoma.

Mtoto Zuwena Bihumo, (14) ambaye ndiye alikuwa akifanyia kazi kama mtumishi wa ndani kwa mama huyo, anadaiwa kuwa Oktoba 23, 2023; alifariki dunia baada ya kupigwa viboko na bosi wake, ambavyo vinadaiwa kumsababishia majeraha mbalimbali mwilini, ambayo ndiyo kiini cha kifo chake.

Hayo yamebainishwa Oktoba 26, 2023 na jeshi hilo, huku likisema kuwa baada ya kifo hicho, mwanamke huyo anadaiwa kutoroka na kwamba juhudi za kumatafuta zinaendelea, japo mumewe yuko mikononi mwa Polisi.

Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Simon Maigwa amesema: "Tunamshikilia mtuhumiwa mmoja mwanaume (Jina limehifadhiwa kwa sababu za kiuchunguzi) kwa kudaiwa kusababisha kifo cha binti aitwaye Zuwena Bitaliho Bihumo, (14) mfanyakazi wa ndani mwenyeji wa Kigoma."

"Mtuhumiwa huyo na mke wake walikuwa wakimfanyia ukatili binti huyo kwa kumchapa na kitu kinachodhaniwa ni fimbo maeneo mbalimbali ya mwili wake na kupelekea majeraha makubwa yaliyosababisha kifo chake," ameongeza Kamanda Maigwa.

Kamanda huyo amesema baada ya kutenda unyama huo, ‘waajiri’ hao walimfikisha marehemu Hospitali ya Wilaya ya Hai kama mgonjwa huku wakitambua kuwa alishafariki muda mrefu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live