Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

House girl akamatwa na dawa za kulevya

109ed027 8a81 48fe 9d90 88955729e079 660x400.jpeg House girl akamatwa na dawa za kulevya

Mon, 28 Sep 2020 Chanzo: millardayo.com

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini imemkamata Maria Edson Mtambo (25) Mnyiha na mkazi wa Tegeta kwa Ndevu akiwa anasafirisha dawa za kulevya aina ya Heroin zenye uzito wa gramu 448.12 kuelekea nchini India, dawa hizo alizihifadhi katika kifurushi cha vitabu viwili ambavyo ndani yake kuliwekwa unga wa dawa hizo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamishina Jenerali wa Mamlaka hiyo James Kaji amesema kuwa binti huyo ni mfanya usafi huko Tegeta na aliyekuwa anamtumia dawa hizo ni mpenzi wake raia wa nje.

Kaji amewataka vijana kuwa makini na raia wa nchi za Magharibi kwa usalama zaidi.

TAZAMA VIJANA 997 WAKIHITIMU MAFUNZO YA AWALI YA KIJESHI

Chanzo: millardayo.com