Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

‘House boy’ auawa madai ya kuua watoto wa bosi wake

Crime Scene Decoration  Mw 133583 2 ‘House boy’ auawa madai ya kuua watoto wa bosi wake

Fri, 10 Jul 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

WATOTO wawili wa familia moja wanadaiwa kuuawa na kijana wa kazi za ndani kisha na yeye kuuawa na wananchi waliokuwa na silaha mbalimbali.

Tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa moja usiku katika Kijiji Cha Kwazoka Wilaya ya Kipolisi Chalinze mkoani Pwani.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa, alisema tukio hilo limefanywa na Yasin Abdalla (35), mfanyakazi wa ndani wa Wema Senzie ambaye aliwaua watoto wawili kwa kuwakata na mapanga na kumjeruhi mama yao, Saada Salehe (28).

Kamanda Wankyo aliwataja watoto waliouawa kuwa ni Rehema Makolo (5) mwanafunzi wa awali na Abubakar Makolo(6) darasa la kwanza, wote walikuwa wanasoma katika Shule ya Msingi Kwazoka.

Akielezea tukio hilo, alisema baada ya mtuhumiwa kufanya tukio hilo la mauaji, wananchi walimkamata na kumuhifadhi katika ofisi ya kijiji, na kuwa akiwa humo alivunja mlango na kukimbia, lakini wananchi walifanikiwa kumkamata na kumshambulia kwa silaha za jadi na kufariki papo hapo.

Kamanda huyo alisema majeruhi ambaye ni mama wa watoto hao, amelazwa katika Kituo cha Afya Mlandizii qkipatiwa matibabu, huku maiti zikihifadhiwa katika kituo hicho kusubiri taratibu za mazishi.

Kamanda alisema uchunguzi wa tukio hilo unaendelea, na kwamba taarifa za awali za kiuchunguzi kuhusiana na mauaji hayo zinaelezwa kuwa kulikuwa na ugomvi kati ya mama wa watoto hao na mtuhumiwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live