Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

'House Boy' ahukumiwa kunyongwa kwa kumuua boss wake

HUKUMU 'House Boy' ahukumiwa kunyongwa kwa kumuua boss wake

Tue, 14 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mfanyakazi wa ndani wa kiume 'house boy', Ismail Sang'wa (28), amehukumiwa kunyongwa hadi kufa baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kumuua kwa kumkata shingo na panga aliyekuwa mwajiri wake, aliyekuwa Ofisa wa Intelijensia wa Shirika la Hifadhi za Taifa nchini (TANAPA ), Emily Kisamo (52).

Hukumu hiyo ilitolewa jana Machi 13,2023 na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Jaji Joachim Tiganga aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo.

Katika kesi hiyo ya mauaji namba 70/2022, upande wa Jamhuri uliwakilishwa na mawakili wa Serikali wandamizi Janeth Sekule, Grace Madikenya na Charles Kagirwa huku mtuhumiwa huyo akitetewa na Wakili Victor Benard.

Akisoma hukumu hiyo Jaji Tiganga, alieleza mahakama imemtia hatiani mtuhumiwa huyo baada ya kuthibitika alimuua kwa makusudi Kisamo ambaye alikuwa mwajiri wake kinyume na vifungu vya 196 na 197 vya Sheria ya Kanuni ya Adhabu na kumhukumu kunyongwa hadi kufa.

Pia, alieleza kuwa kupitia ushahidi wa Jamhuri umeweza kuthibitisha mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo Desemba 18,2015 nyumbani kwa marehemu eneo la Uzunguni jijini Arusha majira ya asubuhi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live