Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hoja ya mashahidi wanapaswa kulipwa lini wakwamisha kesi ya Gugai

Wed, 19 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam imeshindwa kuendelea na ushahidi kwa zaidi ya mara tatu katika kesi ya utakatishaji fedha na kumiliki mali zilizozidi kipato halali, inayomkabili aliyekuwa Mhasibu Mkuu wa Takukuru, Godfrey Gugai na mwenzake baada ya upande wa mashtaka kudai hawajaleta mashahidi kutokana na mahakama hiyo haina fedha ya kuwalipa.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Awamu Mbagwa amedai leo Jumanne Juni 18, 2019 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa shauri lilikuja kwa ajili ya kuendelea na ushahidi lakini wameshindwa kuwaleta mashahidi kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na hela ya kuwalipa.

Baada ya maelezo hayo Hakimu Simba amesema washtakiwa hao wamekaa muda mrefu mahabusu hivyo upande wa Jamhuri muhakikishe mnawaleta mashahidi siku ya shauri hilo.

Hakimu Simba baada ya kutoa maagizo hayo  majibu yakawa kama hivi;

Wakili Mbangwa: Upande wa mashtaka hatujaleta mashahidi kwa sababu mahakama haijatoa fungu.

Hakimu Simba: Mimi ninavyojua shahidi analipwa baada ya kutoa ushahidi hivyo mnatakiwa kutoa wito wa kuwaita  mahakamani.

Pia Soma

Wakili Mbangwa: Nimeieleza mahakama hii kuwa hatuna mashahidi sababu mahakama haina hela ya kuwalipa  na mahakama hii ilitujibu haina fedha ya kuwalipa hivyo hatuwezi kuandaa wito wa kuwaita wakati fedha ya kuwalipa hatuna.

Hakimu Simba: Napanga Juni 20 na Juni 25,2019 kesi itaendelea na ushahidi hivyo naomba upande wa mashtaka muendelee kufanya mawasiliano.

Wakili Mbagwa: Mahakama hii ilituandikia barua ikieleza kuwa fedha haina  mashahidi waje halafu wasubiri watalipwa.

Mbali na Gugai, washtakiwa wengine katika kesi hiyo, ni George Makaranga, Leonard Aloys na Yasin Katera.

 

Katika kesi ya msingi Gugai na mwenzake wanakabiliwa na makosa 43, kati ya hayo, makosa 19 ni ya kughushi, 23 ni utakatishaji fedha na moja ni kumiliki mali zilizozidi kipato halali, ambalo linamkabili Gugai.

Gugai anakabiliwa na kosa la kumiliki mali kinyume na kipato chake, ambapo alitenda kosa hilo kati ya January 2005 na Decembea 2015.

Inadaiwa kuwa akiwa Takukuru Dar es Salaam, Gugai alikuwa akimiliki mali za zaidi ya Sh3.6 bilioni ambazo hazilingani na kipato chake huku akishindwa kuzitolea maelezo.

Chanzo: mwananchi.co.tz