Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

‘Helmet’ zawasweka ndani siku 28

11084 HELMET+PIC TanzaniaWeb

Thu, 9 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Tanga. Jumla ya watu 23 wamefungwa kifungo cha siku 28 jela kwa makosa ya kutovaa kofia ngumu maarufu ‘helmet’.

Kadhalika wazazi saba waliobainika kusafirisha watoto wao chini ya miaka tisa kwa kutumia usafiri wa bodaboda.

Bodaboda hizo zimedaiwa kutumika kama usafiri wa kupeleka wanafunzi shuleni, huku zikipakia zaidi ya mmoja ikiwa ni kinyume cha sheria ya leseni za usafirishaji.

Akizungumza leo Agosti 9 na Mwananchi, Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani mkoa wa Tanga, (RTO) Solomon Mwangamilo amesema operesheni hiyo ya mwezi mmoja imesaidia kurudisha nidhamu ya utii wa sheria bila shuruti katika mkoa huo.

Amesema sheria ya leseni za usafirishaji namba 317 tangazo la serikali 419 inamtaka kila dereva na abiria wake wavae kofia ngumu.

“Watu 23 wapo jela, tumekuwa tukichukua hatua ya kuwaandikia faini kesho wanarudia kosa lilelile kwa hiyo tukakubaliana na wenzetu  tukaanza kuwafikisha mahakamani kwa kesi hizo,” amesema.

Amesema suala hilo limeleta matokeo chanya kwa mkoa huo wa kipolisi, hali inayomfanya kila abiria na dereva wake kuvaa kofia ngumu wakati wote.

“Nia ni kuhakikisha kwamba kila mmoja anavaa kofia ngumu hata akipata tatizo anakuwa salama , hospitali ya Bombo madaktari wa mifupa wapo wengi tu mtu akivunjika mfupa au mguu atatibiwa lakini akiumia kichwa inakuwa ni shida hivyo bila udhibiti wa kutumia helmeti madhara ni makubwa,” amesema RTO huyo.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz