Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hekari 8 za Bangi za fyekwa tena Arusha, Viongozi watatu wa Serikali wanatafutwa

3022 Bangi 2 660x400

Mon, 12 Feb 2018 Chanzo: millardayo.com

Leo February 10,2018 Katibu Tawala wa wilaya ya Arumeru Timotheo Mzava akishirikiana na Jeshi la Polisi pamoja na Watendaji wa serikali wamefika katika kijiji cha Losinoni juu kilichopo Arumeru nakukuta mashamba makubwa ya bangi yakiwa yamechanganywa na Mahindi pamoja na Maharagwe.

Akiongea baada ya zoezi hilo Mzava ameagiza Watendaji wote wa Serikali ikiwemo Mtendaji wa Kijiji kukamatwa kwa kuhusika na kilimo hicho.

“Tumefyeka hekari 8 mpaka saivi hatujamaliza na hatujui tutamaliza saa ngapi, imelimwa kwa wingi imechanganywa kwenye mahindi na maharage, tumetoa maelezo kuanzia Mwenyekiti ambaye tutakuta Kijiji chake kinalimwa Bangi tutamchukulia hatua,” -Katibu Tawala Mzava

ALICHOZUNGUMZA KIBATALA BAADA  YA SUGU KUACHIWA, AMETAJA KILICHOKUWA KINAKWAMISHA DHAMANA

Chanzo: millardayo.com