Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hatima ya Seth mikononi mwa DPP

Ruge Habinda Hatima ya Seth mikononi mwa DPP

Fri, 4 Jun 2021 Chanzo: ippmedia.com

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon, alidai hayo jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi, wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa na kujua hatua iliyofikia katika mazungumzo hayo.

Kesi hiyo iliyokuja kwa ajili ya kutajwa, upelelezi wake haujakamilika na mazungumzo yaliyokuwa yakifanyika kwa ajili ya kumaliza kesi dhidi ya mshtakiwa Seth yanaendelea pale yalipoishia, yakisubiri mwongozo kutoka kwa DPP mpya aliyeteuliwa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Mshtakiwa Seth na Wakili Joseph Makandege, waliwasilisha ombi kwa DPP wakionesha nia yao ya kutaka kumaliza kesi kwa kukiri makosa yao lakini, Mei 6, mwaka huu, Wakili Makandege, aliondoa nia yake ya kufanya mazungumzo na DPP akieleza kwamba mazungumzo hayo hayana afya na yamechukua muda mrefu kukamilika.

Mbali na Seth washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni mfanyabiashara James Rugemalira na wakili Makandege

Rugemarila, ambaye ni Mkurugenzi wa VIP na mmiliki mwenza wa zamani wa IPTL na Seth ambaye ni Mwenyekiti Mtendaji wa PAP, wanadaiwa kutenda makosa hayo katika Jiji la Dar es Salaam na nchi za Afrika Kusini, Kenya na India.

Washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka 12 yakiwamo ya utakatishaji fedha, miongoni mwa mashtaka hayo yapo ya kula njama, kujihusisha mtandao wa uhalifu, kughushi na kutoa nyaraka za kughushi na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, kutakatisha fedha na kusababisha hasara ya Dola za Marekani 22,198,544.60 na Sh. 309,461,300,158.27.

                                                

Wanadaiwa kati ya Oktoba 18, mwaka 2011 na Machi 19, mwaka 2014 jijini Dar es Salaam walikula njama katika nchi za Afrika Kusini, Kenya na India ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Mwanasheria Makandege, anakabiliwa na mashtaka matano likiwamo la kuisababishia serikali hasara ya Dola za Marekani 980,000.

Chanzo: ippmedia.com