Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hatima dhamana ya mbunge Kishapu kesho

Kishapu Hatima dhamana ya mbunge Kishapu kesho

Thu, 14 May 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MAHAKAMA Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga, imeanza kusikiliza maombi ya dhamana dhidi ya kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mbunge wa Jimbo la Kishapu, Suleiman Nchambi, baada ya Mahakama ya Wilaya ya Shinyanga kutokuwa na uwezo wa kutoa dhamana kesi za uhujumu uchumi.

Maombi hayo yalianza kusikilizwa jana katika mahakama hiyo chini ya Jaji Phocus Mkeha. Wakili wa mbunge huyo, Frank Mwalongo, alidai baada ya mahakama hiyo kutokuwa na uwezo wa kusikiliza kesi za uhujumu uchumi ilibidi waombe dhamana kwenye Mahakama Kuu.

Jaji Mkeha alisema uamuzi ya utoaji wa dhamana hiyo atatoa Mei 15.

Mei 11, mwaka huu Mahakama ya Wilaya ya Shinyanga, ilishindwa kutoa dhamana ya mbunge huyo, kwa maelezo kuwa haina uwezo wa kusikiliza kesi za uhujumu uchumi wala utoaji wa dhamana kwa makosa yasiyozidi Sh. milioni 10, hati ya mashitaka ya mbunge huyo haijataja thamani na kuambiwa waombe dhamana kwenye Mahakama Kuu.

Mbunge huyo kwa mara ya kwanza alipandishwa kizimbani Mei 8, mwaka huu katika Mahakama ya Wilaya ya Shinyanga na kusomewa mashitaka 12 ya uhujumu uchumi kwa kumiliki silaha na risasi kinyume cha sheria.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live