Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Haonga aripoti polisi, aachiwa bila masharti

56580 Haonga+puic

Fri, 10 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Mbunge wa Mbozi (Chadema),  Pascal Haonga ametakiwa kutoripoti tena polisi hadi watakapomuita au akiambia vinginevyo.

Akizungumza na Mwananchi Digital leo Alhamisi Mei 9, 2019 katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Haonga amesema mapema leo alikwenda kituo cha polisi kama alivyotakiwa lakini hakusumbuliwa wala kuandika maelezo bali aliambiwa afanye shughuli zake wakimhitaji watamuita.

Haonga alikamatwa mwanzoni mwa wiki hii kwa kile alichoelezwa kutenda makosa ya kimtandao na kuwekewa dhamana na Mbunge wa Rombo (Chadema), Joseph Selasini.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Giles Muroto, alithibitisha kukamatwa kwake lakini akasema wamemuachia kwa dhamana huku akitaja kosa la kushilikiliwa kwake ni makosa katika matumizi ya mtandao.



Chanzo: mwananchi.co.tz