Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hans Poppe, Lauwo wafikishwa mahakamani

22487 Hans+pic TanzaniaWeb

Wed, 17 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa kamati ya Usajili ya klabu ya Simba, Zacharia Hans Poppe na mfanyabiashara Franklin Lauwo wamefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Jumanne Oktoba 16, 2018  saa 3:30 asubuhi.

Hans Poppe na Lauwo baada ya kufikishwa mahakamani hapo wamepelekwa moja kwa moja katika chumba cha mahabusu wakisubiri kupandishwa kizimbani.

Mwenyekiti huyo wa usajili wa Simba amefikishwa mahakamani hapo siku moja baada ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kukiri kumkamata ikiwa ni baada ya kumtangaza katika vyombo vya habari na kumtaka aripoti katika ofisi zake ili kujibu tuhuma zinazomkabili.

Alikamatwa juzi baada ya kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), saa 8:59 mchana akitokea Dubai.

Pamoja na Hans Poppe, mwingine aliyekuwa anatafutwa na Takukuru ni Lauwo ambaye naibu mkurugenzi wa Takukuru, Brigedia Jenerali John Mbungo aliieleza MCL Digital kuwa alikwishawasiliana naye na kudai atajisalimisha mwenyewe mara baada ya kurejea nchini akitokea Pakistan.

Wawili hao wataunganishwa katika kesi inayomkabili rais wa Simba, Evans Aveva  na makamu wake, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ ya madai ya kughushi na utakatishaji fedha ambayo inaendelea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.

Hans Poppe amekamatwa na kufikishwa mahakamani zikiwa zimepita siku 31 tangu Takukuru ilipojitokeza mbele ya waandishi wa habari kumtaka yeye na Lauwo wajisalimishe huku wakitangaza dau kwa yeyote ambaye atafanikisha kukamatwa kwao.

Soma Zaidi:

Takukuru yamnasa Hanspoppe Uwanja wa Ndege Dar

Endelea kufuatilia MCL Digital kwa taarifa zaidi

Chanzo: mwananchi.co.tz