Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Halima Mdee ahojiwa na polisi

9632 Pic+mdee TanzaniaWeb

Thu, 2 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mbunge wa Kawe, Halima Mdee, wanachama na wafanyabiashara wamehojiwa na polisi wa kituo cha Kawe, kwa kosa la kufanya mkutano bila kibali.

Akizunguma na MCL Digital leo Agosti Mosi, Mdee amesema alipigiwa simu na vijana wanaofanya biashara ya kutengeneza bustani wa eneo la Mzimuni, Kawe kwamba wamepewa notisi ya kuondoka.

Amesema wakati anapigiwa simu, alikuwa Kunduchi katika ziara hivyo ikamlazimu kwenda kuwasikiliza wananchi wake.

“Nilipofika, nilizungumza nao na kuwaeleza suala hili nalishughulikia, kwani nimewasiliana na wizara ya ardhi, mipango miji na Tarura (wakaka la wabarabara za vijijini na mijini).”

“Ni kweli wale vijana wako eneo la barabara na wamenieleza hawana tatizo la kuondoka, lakini wanahitaji kuelekezwa wapi watakwenda kuendelea na shughuli zao.” amesema.

Amesema baada ya kumaliza kuzungumza nao, aliondoka lakini alipofika mbele akaelezwa kuna watu wamekamatwa huko alipotoka.

“Nikaona nirudi, nilipofika nikakuta baadhi ya wafanyabiashara na wanachama wanarushwa kichura chura, nikahoji kuna nini sikupata majibu yanayoeleweka.”amesema.

Mdee amesema baada ya hapo, watuhumiwa hao waliokuwa chini ya ulinzi, wakapelekwa kituo cha polisi Kawe  na yeye akatangulia kituoni.

“Nilipokuwa nakwenda, kama mita 20 nikaambia na mheshimiwa rudi, niliporudi nikaambiwa niko chini ya ulinzi, na kuniweka katika gari yao, tukaenda hadi kituoni na kuhojiwa kwa kufanya mkusanyiko usiokuwa na kibali,” amesema Mdee

Hata hivyo, baada ya kuhojiwa wale wafanyabiashara na wanachama wa Chadema  waliachiwa  huru.

Akizungumzia suala hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni,Jumanne Murilo alisema kazi ya jeshi la Polisi ni kutoa huduma za kiusalama kwa mtu yeyote hivyo si ajabu kwa kiongozi wa chama kufika katika kituo cha Polisi inapobidi.

“Mtu yeyote akifika kituoni ina maana amekamatwa?huyo Makene au Mbowe au Mdee akifika kituoni maana yake amekamatwa?hilo ndilo swali langu,”amehoji.

“Hivyo watu wasitumie Jeshi la Polisi kujipatia umaarufu,”amesisitiza.

Chanzo: mwananchi.co.tz