Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Halima Mdee, Boniface Jacob na wenzao 26 waachiwa huru

46731 MATIKO+PIC Halima Mdee, Boniface Jacob na wenzao 26 waachiwa huru

Thu, 6 May 2021 Chanzo: millardayo.com

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeifuta kesi ya wafuasi  27 wa CHADEMA wakiwemo Wabunge watatu waliokuwa wanakabiliwa na mashtaka ya kufanya mkusanyiko na kutotii amri halali katika geti la gereza la Segerea.

Washtakiwa hao wamefutiwa kesi hiyo na kuachiwa huru Jumatano May 5, 2021 na Mahakama hiyo baada ya upande wa mashtaka kushindwa kupeleka mashahidi Mahakamani kwa ajili ya usikilizwaji wa shauri hilo.

Uamuzi wa kuwafutia kesi hiyo umetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Huruma Shaidi wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya kuanza usikilizwaji.

Hakimu Shaidi ameifuta kesi hiyo baada ya upande wa mashtaka kushindwa kupeleka mashahidi kwa muda mrefu. Miongoni mwa washtakiwa katika kesi hiyo ni Mbunge wa Viti Maalum, Halima Mdee na Wabunge wenzake, Ester Bulaya na Esther Matiko.

Mbali na Wabunge hao, washtakiwa wengine ni, aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob, Patrick Assenga, mfanyabiashara, Henry Kilewo na wengine 21.

Kabla ya kufutwa kwa kesi hiyo, Wakili wa Serikali mwandamizi, Mkunde Mshanga amedai kuwa shauri hilo liliitwa kwa ajili ya kuendelea na usikilizwaji wa ushahidi lakini upande wa mashtaka hawakuwa na shahidi na kuiomba mahakama hiyo ipange tarehe nyingine kwa ajili ya kusikilizwa.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka,  washtakiwa kwa pamoja wanadaiwa kutotii amri halali iliyotolewa na askari Magereza  tukio wanalidaiwa kutenda Machi 13, 2020 eneo la gereza la Segerea lililopo wilaya ya Ilala.

Siku hiyo ya tukio, washtakiwa kwa makusudi walikaidi amri halali ya kuondoka eneo la gereza kwa amani ili eneo hilo libaki wazi, amri hiyo iliyotolewa na askari mwenye namba B 3648 sajenti John ambaye ni mlinzi wa geti la gereza hilo.

BILA KUPEPESA MACHO RAIS SAMIA ANENA “TUNAVAA BARAKOA KAMA MBUZI, CORONA NI JANGA”

Chanzo: millardayo.com