Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hakimu, mawakili wakwamisha kesi ya Gugai

33669 Takukuru+pic Tanzania Web Photo

Thu, 27 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mawakili wa utetezi katika kesi ya utakatishaji fedha na kumiliki mali zilizozidi kipato chake  inayomkabili aliyekuwa mhasibu mkuu wa Takukuru,  Godfrey Gugai wamekwamisha kuendelea kwa kesi hiyo baada ya kutotokea mahakamani.

Wakili wa Takukuru, taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa, Vitalis Peter ameeleza hayo leo Alhamisi Desemba 27, 2018 mbele ya hakimu mkazi mkuu, Janeth Mtega kuwa kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kuendelea na usikilizwaji lakini mawakili wa utetezi na hakimu anayesikiliza kesi hiyo hawapo.

“Kesi iko hatua ya usikilizwaji imekuja kwa ajili ya kuendelea na ushahidi lakini wakili wa utetezi na hakimu anayesikiliza kesi hii hawapo hivyo tunaomba tarehe nyingine,” amedai Peter.

Baada ya maelezo hayo Hakimu Mtega ameahirisha kesi hiyo hadi Januari 10, 2019.

Tayari mashahidi sita wa upande wa mashtaka wameshatoa ushahidi wao dhidi ya Gugai.

Gugai na wenzake watatu wanakabiliwa na mashtaka 43, kati ya hayo, 19 ni ya kughushi, 23 ni utakatishaji fedha na moja ni kumiliki mali zilizozidi kipato halali ambalo linamkabili Gugai.

Mbali na Gugai, washtakiwa wengine ni George Makaranga, Leonard Aloys na Yasin Katera.

 

 



Chanzo: mwananchi.co.tz