Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hakimu atishia kuifuta kesi ya Halima Mdee kisa...

68911 Pic+mdee

Tue, 30 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam imesema itaifuta kesi ya kutoa lugha chafu dhidi ya Rais wa Tanzania, John Magufuli inayomkabili mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee kwa sababu ya shahidi kushindwa kutoa ushahidi wake kwa zaidi ya mara tatu mfululizo.

Hayo yamesemwa leo Jumanne Julai 30,2019 na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Thomas Simba baada ya Wakili wa Serikali, Silivia Mitato kudai wakili anayeendesha shauri hilo amepangiwa kazi nyingine hivyo anaiomba mahakama impe muda ili apitie jalada hilo.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Simba amesema kumbukumbu zake zinaonyesha shahidi Abdull Chembea amefika mahakamani hapo zaidi ya mara tatu na hajawahi kutoa ushahidi.

"Hili shauri mimi nitalifuta kwa kuwa shauri hili lipo tangu mwaka 2017 kila nikija namuona huyu shahidi anakuja lakini hakuna kinachoendelea, naona upande wa mashitaka mnakwamisha shauri lisiendelee, nawapa sharti mtakapokuja awamu ijayo nataka shauri hili liendelee," amesema.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 28 na Septemba 4, 2019 kwa ajili ya kusikilizwa.

Hadi sasa mashahidi watatu wa upande wa mashtaka wameshatoa ushahidi akiwemo mkuu wa kituo cha polisi cha Urafiki, mrakibu wa Polisi (SP), Batseba Kasanga.

Pia Soma

Katika kesi ya msingi inadaiwa Julai 3, 2017 katika ofisi za makao makuu ya Chadema zilizopo mtaa wa Ufipa wilayani Kinondoni, Dar es Salaam, Mdee alitamka maneno dhidi ya  Rais Magufuli kuwa,  “anaongea hovyo, anatakiwa  afungwe breki”,  kitendo kinachodaiwa kuwa ni kumdhalilisha Rais na kusababisha uvunjifu wa amani.

Chanzo: mwananchi.co.tz