Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hakimu ataka upelelezi kukamilika kesi ya Shamimu, mumewe

77491 Pic+shamimu

Sat, 28 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeutaka upande wa mashtaka kukamilisha upelelezi wa kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili, Abdul Nsembo maarufu Abdulkandida na mkewe, Shamim Mwasha.

Hatua hiyo imefikiwa leo Septemba 26,2019 na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Kelvin Mhina baada ya wakili wa utetezi,  Charles Kisoka kuomba upelelezi wa kesi hiyo kuharakishwa ili ukamilike kwa wakati.

SOMA ZAIDI: Kesi ya Shamim, mmewe mambo ni yaleyale

Awali, wakili wa Serikali mwandamizi, Wankyo Saimoni amedai mahakamani hapo kuwa kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kutajwa upelelezi bado haujakamilika.

Hakimu Mhina ameahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 11, 2019 kwa ajili ya kutajwa na washtakiwa wamerudishwa rumande.

Shamimu ambaye ni mmiliki wa Blog 8020 Fashion na mumewe wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi namba 36/2019.

Pia Soma

Advertisement

SOMA ZAIDI: Kesi ya Shamimu na mumewe, Mahakama inasubiri ripoti ya Mkemia Mkuu

Washitakiwa hao ambao ni wakazi wa Mbezi Beach, walifikishwa kwa mara ya kwanza mahakamani  Mei 13, 2019.

Wawili hao walifikishwa mahakamani hapo wakikabiliwa na mashitaka ya uhujumu uchumi ambayo ni kusafirisha dawa za kulevya aina ya Heroin Hydrochloride zenye uzito wa gramu 232.70.

Inadaiwa Mei Mosi, 2019 wakiwa Mbezi Beach Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam walisafirisha dawa hizo.

SOMA ZAIDI: Kilichojiri kesi ya Shamimu, mume wake hiki hapa

Chanzo: mwananchi.co.tz