Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hakimu ataka upelelezi kesi ya Ayub Kiboko na mkewe ukamilike

Tue, 17 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam.Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu , Thomas Simba ameutaka upande wa mashtaka kuhakikisha wanafuatilia upelelezi wa kesi ya kukutwa na dawa za kulevya inayomkabili, Ayub Kiboko na mkewe, Pilly Mohamed kwa kuwa shauri hilo lipo mahakamani kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Wakili wa Serikali, Silvia Mitanto alidai kuwa shauri lilikuja kwa ajili ya kutajwa na upelelezi bado haujakamilika.

Baada ya maelezo hayo Hakimu Simba amesema tangu washtakiwa hao wafikishwe mahakamani hapo kesi hiyo imeshafikisha  mwaka mmoja na miezi mitatu upelelezi bado haujakamilika hivyo aliwataka mfuatilie mjue umefikia wapi.

"HiI kesi ina mwaka mmoja na miezi mitatu nataka shauri hili litakapokuja tena mahakamani mtupe jibu sahihi mfuatilie upelelezi umefikia wapi,” amesema Simba.

Shauri hilo limeahirishwa hadi Septemba 30, 2019.Kiboko na mkewe wanakabiliwa na shtaka moja Katika kesi ya uhujumu uchumi namba29/2018, wakidaiwa kusafirisha dawa zabkulevya aina ya heroin yenye uzito wa gramu 251.25

Wanadaiwa Mei 23, 2018 eneo la tegeta Nyuki Masaiti wilaya ya Kinondoni walisafirisha dawa hizo

Pia Soma

Advertisement

Chanzo: mwananchi.co.tz